AFANDE SELE AWATUPIA MANENO CHADEMA
AFANDE SELE AWATUPIA MANENO CHADEMA
ni flani kashika kipaza sauti........ Kwajina la kuzaliwa anaitwa SELEMAN MSINDI ila kwa jina la jukwaani anajulikana kama afande sele.. Wiki iliyopita alitoa shutuma dhida ya chama cha demakrasia na maendeleo kwa kusema wanapoteza umaarufu kwa kitu kidogo (pesa). Afandesele anaonekana hajafurahishwa hata kidogo kwa mh LOWASSA kujiunga na chama hicho
aliamuka kusema hivi
"Zamani kidogo kauli mbiu yao ilikuwa Peaples power lakini sasa hivi kauli mbiu yao ni ten billiooons power,tamaa ya pesa na uchu wa madaraka imewafanya wanunuliwe .Eti leo wanasema Lowasa safiiii,Mtu mliye mtusi kwa miaka minane mnataka kumsafisha kwa miez miwili kama si foolishness ni nini?eti bila aibu yanajitetea ooh Kama kweli ni fisadi mbona hajashitakiwa mahakamani. Huu ni zaidi ya ujinga wanaotoa utetezi huo wengine maprofesa na wengine wanasheria tena wakubwa tu,sasa katika hali ya kawaida tu aliyetukana na aliyetukanwa nani anapaswa kwenda mahakamani?Dk Slaa(Mzee muadilifu na Mzalendo wa kweli alishawahi kusema mara nyingi tu kuwa Lowasa ni fisadi papa na Kama haitoshi slaa huyohuyo kuwa kama Lowasa anabisha kuwa yeye si fisadi papa aende mahakamani kumshitaki Slaa mpaka leo Lowasa hajawahi kwenda mahakamani angalau kulalamika matusi hayo. Watanzania ufike wakati tujiondoe katika mawazo mgando. Msikubali kugeuzwa kama Chapati."