LYRICS NAY WA MITEGO WAPO
LYRICS: NAY WA MITEGO WAPO
Verse 1:
Unachokipanda leo ndicho utachovuna kesho.Imeandikwa Mwanaume kula kwa jasho.
Najiuliza hivi ni nani kaiona kesho.
Chapa mwendo na ukilala hauna chako.
Hivi uhuru wa kuongea kwenye hii nchi bado upo?.
Usije kuongea vitu kesho ukajikuta sentro.
Chorus:
Kuna viongozi wavuta bangi? "wapo "Maana wana maamuzi ya kise.... "wapo"
Kuna walio mmiss Jakaya? "wapo"
Walio choka kuisoma namba? "wapo"
Kuna walio poteza malinda? "wapo"
Kuna wasanii mateja? "wapo"
Kuna mademu wanasagana? "wapo"
Kuna vidume wanalelewa? "wapo"
Kuna wasanii wanarogana? "wapo"
DOWNLOAD AUDIO BELOW
Verse 2
Kuna Radio na Tv, naona zimeshapoteza CV.Hakuna uhuru wa habari, wala taarifa ya habari.
Wanapindisha pindisha tu kuiogopa serikali.
Siamini nchi inaendeshwa na kiki.
Siasa inafunika mziki.
Viongozi wanashindana kukiki.
Wanagombea front page, wauze kwenye gazeti.
Nasikia kuna viongozi wamefoji vyeti.
Verse 3
Kiongozi mwenye busara anapokea ushauri.Anapokea mawazo,haweki mbele kiburi.
Hey! Samahani mheshimiwa, hivi unamjua BASHITE?.
hili ni jipu jipya toka koromije.
Limesha iva na usaa, limeshatunga.
Na kukabidhi sindano ya kulidunga.
Daktari haogopi ukubwa wa kidonda.
We_si Dr wa majipu, tumbua hakuna kuvunga.
Kuvamia ofisi za watu kumbe nayo ni kazi.
Hakuna noma wanangu pigeni kazi.
Boda boda kazi, bajaji Kazi.
Eti! Vipi? Kukaba nayo kazi?.
Refa ni wao piga manati.
Vita ya Masai na mmang'ati.
Biashara ya ngono na Super shafti.
Pumzi imekata nashika shati...
Hahahahahaha! Wewe mtu gani sasa......
Hutaki kushauriwa, hutaki kukosolewa......
Umerongwa wewe,........
unajiona ndugu yake na Yesu ee....
Oya! Wanangu eeeh! Round hii mtanyooka haki ya Mungu.
Naona kichaa kapewa Rungu..