Utafiti wa ‘TWAWEZA’ umeonesha CCM ina nafasi kubwa zaidi ya kushinda uchaguzi 2015
Matokeo ya utafiti huo yametolewa leo jijini Dar es salaam ambapo yameonesha pia kuwa wagombea wa CCM katika ngazi zote ikiwa ni pamoja na ubunge na udiwani CCM inaongoza. Utafiti huo umeonesha majibu mbali mbali kama ifuatavyo:
Changamoto kubwa za wananchi
Wananchi wengi wanazikumbuka ahadi za wambunge wao lakini wanadai hazijatekelezwa
Ni asilimia 57 tu ya wananchi walioweza kutaja tarehe sahihi ya uchaguzi wa mwaka huu (25 October)
Wananchi wengi walikerwa na foleni ndefu wakati wa uandikishaji wa vitambulisho vya kupigia kura (BVR)
Endapo uchaguzi ungefanyika leo wananchi wangempigia nani, Udiwani
Endapo uchaguzi ungefanyika leo wananchi wengi wangempigia nani, Ubunge
Endapo uchaguzi ungefanyika leo wananchi wangempigia nani, Uraisi
Chama kilicho karibu zaidi na wananchi
Wananchi waliowengi wanaamini ‘UKAWA’ ni chama cha siasa kilichosajiliwa
Uchaguzi ungefanyika leo, wananchi wangempigia mgombea gani
Magufulu Vs Lowasa wanavyopendwa na makundi mbalimbali, Lowasa anapendwa zaidi ni wanaume wakati Magufuli anapendwa zaidi na wanawake
Lowasa Vs Magufuli wanavyokubalika na rika/watu wa umri mbalimbali
Lowasa Vs Magufuli anavyokubalika na watu wenye viwango mbalimbali vya elimu
TWAWEZA ni taasisi isiyo ya kiserikali inayofanya uchunguzi kwa kina katika nyanja mbalimbali hapa Tz na uchunguzi wao ulianza tangu mwaka 2012, mwaka huu umefanya utafiti wao juu ya uchaguzi mkuu tangu mwezi wa nane kwa njia ya simu, uso kwa uso, akitoa ufafanuzi huo Mkurugenzi mtendaji wa Twaweza Aidan Iyekuze
“Utafiti huu sio utabiri wa matokeo ya uchaguzi mkuu, na tulianza kufanya uchunguzi tangu mwezi wa nane mwaka huu na majibu yapo hivi kuanzia nafasi ya:
UDIWANI
CCM 60%
Chadema24%
Cuf 2%
Act wazalendo1%
Nccr mageuzi
UBUNGE
CCm 60%
Chadema 26%
Cuf 3%
Act 1%
Nccr mageuzi 1%
Ukawa 3%
URAIS
CCM 66%
Chadema 22%
Act 0%
Nccr 0%
Ukawa 3%
Utafiti huu tuliufanya kaya kwa kaya.” Aidan Iyakuze