MGOMO WAWALIMU KENYA BADO KITENDAWILI

MGOMO WAWALIMU KENYA BADO KITENDAWILI



Serikali ya Kenya imetangaza kufungwa kwa shule zote za kibinafsi na za umma hadi mgogoro wa walimu wanaogoma wakitaka nyongeza za mishahara utatuliwe. Hatua hiyo imetolewa siku mbili baada ya mahakama kuahirisha hadi tarehe 25 ijumaa ijayo siku ya kutoa uamuzi wa iwapo mgomo huo ni halali au la. 


Wananchi na wazazi kwa ujumla wameeleza hisia zao kutokana na mgomo huo. Wazazi wengi wameitupia lawama serikali kutokana na kuto walipa mishahara walimu hao mpaka inafikia hatua ya kugoma kufundisha. pia ikiwa ni kipindi cha wanfunzi kufanya mitihani ya kumaliza   na wengine kupanda vidato  Hali hii imekua ikijitokeza sana kwenye nchi za maziwa makuu hata hapa Tanzania hali hii imekua kama imeshazoeleka, sababu kubwa ya mgomo huu ni walimu kuishinikiza serikali iongeze mishara yao kwa salimia 50 mpaka 60